Saturday, June 17, 2017

ORODHA/AINA YA WAPENZI


*HII ORODHA YA WAPENZI NI PASUA KICHWA ISEE*

*1. VIPWENTE* - _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Yeye Anaweza Akakumiss Hadi Anahisi Network Zinakatika...Lakini Hakutafuti Ng'ooo Iwe Ni Kwa Message Au Laivulaivu, Kwasababu Hataki Kuonekana Wakwanza Kukutafuta._

*2. VIMBUNDU* - _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Hakuonyeshi Kama Yuko Deep Kwako Hata Kiduchu, Lakini Olewako Akuone Unaongea Na Kidemu/ Kiblazameni Kingine, "Kazi Mbona Unayo"....Hawa Huaga Wanapenda Ndani Kwandani Kama Meli Za Kivita._

*3. VISHOKOMZOBE -* _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Ukihesabu Muda Ambao Mmeanza Kuvunja Amri Ya Sita Yaani Tangu 2014 Mwezi Wakwanza Hadi Lao, Hajawahi Kukupa Hata Kijizawadi Japo Hata Pafyumu Ya Kurusumu._

*4. VINJUNJIO* - _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Yeye Anakuonyesha Tabasamu Pale Tu Anapokabwa Na Ukame,_ _Mkishapandiliana Ukame Ukimuisha Hana Taimu._

*5. ATOMBILE* - _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Yeye Anamichepuko Kama_ _6 Ivi...Lakini Ole Askie Kunamtu Anakunyemelea Wewe, Hio Vitayake Bora World War. Hawa Nao Wanapendaga Ndani Kwandani._

*6. VISHUMUNDU -* _Hawa Ninoma, Ni Aina Ya Wapenzi Ambao We Uwe Na Michepuko, Umpige, Umfungie Nje, Umfokee Kila Mda, Ukatae Kumtambulisha...Yeye Ndo Kwanza Anazidisha_ _Malavidavi...Fanya Ufanyao, Hakuachi Ng'ooo! (Ukikutana Na Wahivi Oa/ Olewa Fasta...Au Hadi Mungu Akwambie Laivu Kwamba Ye Ndo Kakuletea?)_
.
*7. MANDONYA -* _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi _Ambao Yeye Kukuvalisha Pete Sio Kazi Kwake, Tabu Kuoa! Atakuvisha Chuma Lake Utakaa Nalo 3Years, Mwisho_ _Wasiku Unaskia Kamuoa Ntombi Mwakipesile Wa Mtoni Kijichi._

*8. VIBINUZI* - _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Yeye Ukiwanae Muda Wote Anachati, Ukimuuliza Unachati Nanani? Kinawaka._

*9. KIBUMBUSWA -* _Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Yeye Hipiti Siku_ _Hamjagombana. Yani Mnaweza Kwenda Kulala, Ukaweka Pozi La Kulala_ _Kiubavuubavu...Utashangaa Anakwambia,_ _"Yaani Mimi Sipendagi Ukilala Hivo Kwasababu Naota Ndoto_ _Mbayambaya"...Basi Tu Mradi Mgombane._

*10. VITUSU AMAZING* _- Hawa Ni Aina Ya Wapenzi Ambao Mapenzi Yao_ _Yamepitiliza Yaani Nizaidi Ya Mapenzi Ya Mchepuko...Yeye Hata Ukijamba Utaskia,_ _"Pole Baby, Haujaumia?"_
*Kwani We Wako Aina Gani?*

Monday, June 5, 2017

Tangawizi na faida zake


FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni
6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
7. Huondoa maumivu ya koo
8. Huua virusi wa homa
9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini
10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)
14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)
16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo
17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi
19. Huongeza msukumo wa damu
20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo
21. Huzuia damu kuganda
22. Hushusha kolesto
23. Husafisha damu
24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
25. Hutibu shinikizo la juu la damu
26. Husafisha utumbo mpana
27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha
35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
41. Huimarisha afya ya figo
42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha
44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

BLEND KAMA UNAVYO TENGENEZA JUICE YA KAWAIDA KISHA KUNYWA GLASS MOJA KWA SIKU.

AU UNAWEZA KUJENGA MAZOEA YA KUTAFUNA VIPANDE KADHAA KILA SIKU ASUBUHI KABLA HUJALA KITU

@Matahimba

KWA MADIRISHA,MILANGO NA MAGETI YA KISASA

MADIRISHA YA GRILL ZA KISASA
Tofauti na miaka iliyopita ambapo nondo zilitumika kwa kiasi kikubwa, sikuhizi chuma aina ya flat bar na nondo za square bar ndio zmekuwa zikitumika na hakika dirisha zake ziko simple and classic.Teknolojia mpya ya uwekaji grill kwa ndani ya koplo ya dirisha na nje kufuatiwa na frem za dirisha ya aluminium au Upvc imepelekea mvuto wa nyumba zetu kuongezeka na pia thamani kuongezeka kutokana na finishng nzuri ya dirisha.(pichani ni Baadhi ya dirisha za grill za kisasa.Kwa huduma hii wasiliana na workshop yetu kwa 0719911391 kokote tunakufikia)





Thursday, June 1, 2017

Kama PLAY STORE yako inasumbua fanya haya ........




ANDROID MAUJANJA TRICKS JE, Google Play Store yako INASUMBUA? Pata UTATUZI HAPA!
JE, Google Play Store yako INASUMBUA? Pata UTATUZI HAPA


Google Play Store
Google Play Store ni moja kati ya 'APPLICATION' za msingi kwa mtumiaji wa simu janja A.K.A ''Smart Phones''.

>>> Kuna wakati 'Play Store' inakuwa inasumbua, ambapo mtumiaji
anashindwa kufanya vitu mbalimbali kwenye simu yake kama vile ku 'kudownload' applications, au pia kuzi 'update' na pia tatizo la kujifunga 'yenyewe' na kuleta ujumbe wa ''Unfortunately Google has stopped''

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI

1. Force close the Google Play Store
>>Hapa unailazimisha Play store ijifunge. Fanya hivi, nenda Setting > Apps > All halafu ichague Google Playstore halafu click Force stop. Hii inaweza ikamaliza tatizo lililojitokeza awali.



Picha; Force stop au Unistall

2. Zima mtandao kabisa yaani weka 'Airplane mode'
>>Hamna ufanisi sana kwenye njia hii kwa baadhi ya simu lakini hii njia huwa inachagua baadhi ya simu! Kwenye Tecno na Huawei inakubali sana!




3. Cheza na Wifi
>> Jaribu kuzima na kuwasha Wifi kwenye Android yako maana tatizo linaweza likawa ni mtandao wa simu yako.

4. Restart simu yako (Reboot)
>> Kulingana na mpangilio wako wa simu, Restart simu yako ili ku clear cache ambayo pengine inaweza ikawa inasababisha tatizo hilo. Kwa Smart Phone nyingi, ku restart, bonyeza Power button kwa sekunde kama 7 halafu chagua Reboot au Restart kulingana na simu yako! Kwa wengine angalia mpangilio wa simu yako!





5. Futa Google Play Store cache au Data
>> Nenda Setting > Apps > All > Play Store, ichague, halafu click Clear/ Wipe cache na Data kulingana na simu yako!

6. Angalia kwenye 'Disabled Apps'
>> Huenda Play Store ilikuwa imeshitishwa kwenye simu yako, kwa hio lazima uiruhusu kuendelea kufanya kazi! KIVIPI SASA???
>> Nenda Setting >> Apps > All, halafu shuka mpaka chini ambapo Apps zilizokuwa Disabled hukaa, halafu ichague hio Play Store kama ipo hapo, halafu click Enable.





7. Uninstall Google Play Store
>> Fanya kwenda Setting > Apps > All> Play Store, ichague, halafu click Unistall Updates.

8. Ondoa na ingiza Google Account yako
>> Nenda Setting > Accounts na chagua akaunti yako ya google! Halafu gusa kwenye vidoti vitatu, na chagua Remove. Then jaribu kuiingiza Account yako tena kuangalia kama tatizo la Playstore limetatulika!

9. Factory data RESET
>>Baada ya njia zote hizi kufeli, hamna budi kui futa data zote na kuanza upya kabisa! JE, UNAJUA JINSI YA KU ''FACTORY RESET'' simu yako???






>>> Je, wewe huwa unatumia njia ipi kutatua hili tatizo??? Weka comment hapo chini!!

Share :

Facebook Google+ Twitter