SIRI ZINAZOWAFANYA WANAFUNZI KUTOFAULU MITIHANI............
IRI
SIRI ZINAZOWAFANYA WANAFUNZI KUTOKUFAULU MTIHANI ZIKO HAPA
KWANZA kabisa ni kujiamini kupita kiasi, wanafunzi wengi huingia katika dimbwi hili ambapo huamini sana mazoezi ya darasani ambayo wamekwisha ya faulu, huku wakitegemea huenda ikawa sawa na mtihani wa mwisho wa Taifa. Lakini mwanafunzi hupaswi kudharau mtihani wowote kwani mtihani ni mtihani tu hata ukiwa mrahisi kwako, kwani kunasababu za msingi za mtihani huo kutungwa mrahisi.
PILI: Ni kuingia na vikaratasi vya majibu katika chumba cha mtihani. Hii ni sababu kubwa sana kwa wanafunzi wasiopenda kujisomea, na hata kama unaakili kiasi gani au umejisomea kiasi gani, ukishaingia na kikaratasi au majibu uliyoandika mapajani (wasichana) lazima kwanza kile chote ulichokuwa umesoma kifutike kichwani mwako hivyo utaanza kuyategemea majibu uliyojiandika na katika kikaratasi na pia lazima utabaki kuwa ni mtu wa wasi wasi.
Ukishaingia katika hali hii ujue mambo yataharibika tu, kwani utachukua muda mwingi kujibu swali moja lenye maksi ndogo, kuliko yule aliyeingia bila kibuti, nondo, kibomu kwenye mtihani. Kuna uwezekano mkubwa wa mwanafunzi angalau kupata maksi nzuri pale anapoingia kwenye mtihani huku akitegemea akili yake, kwani humpa nafasi ya kutafakari kwa kina na kurejea aliyokwisha jisomea hapo nyuma.
TATU: Wanafunzi hawana utamaduni wa kujisomea kwa kutaka kujua wasiyokuwa wakijua au wasiyokuwa wamefundishwa na mwalimu darasani. Mwanafunzi anatakiwa kuhangaika huko na kule kutafuta pamphlet au kwa lugha zao wanaita "material" kutoka kwa wenzao wa shule za jirani kwani katika mtihani huwezi kuletewa yote uliyojifunza katika vipindi vya darasani. Pia lazima mwanafunzi awe na ratiba nzuri ya kujisome, utakuta mwanafunzi kwasababu anapenda somo la history basi atalisoma kila siku na kuacha masomo mengine.
NNE: Wanafunzi wanakosa maswali ya uelewa yani utashi katika kupambanua mambo ni tatizo kwa wengi na sio kwamba hawawezi, lakini hawana muda wa kufuatilia habari za kitaifa na kimataifa ili waweze kuongeza ufahamu (IQ) wao katika maswala mbali mbali ya kijamii na kiutawala wa nchi. Mwanafunzi anapaswa kufuatilia matukio kadhaa yanayotokea nchini pamoja na mabadiliko ya viongozi wa serikalini; kwa mfano wanapaswa kusikiliza bunge mara wanapopata muda wa mapumziko.
TANO: Mwanafunzi anapaswa kuwa yeye kama yeye na sio kufuata nyendo zote za mtu, ni sawa kufuata yale mazuri jirani yako anayoyafanya lakini kuna mambo ambayo ni personal na sii ya kuiga yakawezekana, kwa mfano; utakuta mwanafunzi fulani anatumia muda mchache sana kujisomea na akaelewa na kushika alichosoma na wengine labda huhitaji muda mrefu kuelewa kitu, je ukimuiga huyo wa muda mfupi utafanikiwa? Unapaswa kujitambua wewe ni mtu wa aina gani kisha ufuate asili yako inavyo sema.
SITA: Mitandao ya kijamii pia ni tatizo kwa wanafunzi wengi, wengine hutumia mitandao hii kurefresh mind (akili) zao lakini wengine muda wote huonekana kuchat na kufungua kurasa za maswala ya uchi, hii kisakolojia lazima ikujengee mazingira tofauti kabisa na maswala ya shule hata kama ni mtu tu wa kawaida ambae hayuko shule lazima itakupa hamasa za kingono tu. Hivyo mwanafunzi atanufaika na mtandao wa internet endapo atautumia muda wake katika mtandao huo kutafuta material ya kusoma, kwani kwa bahati nzuri siku hizi kila kitu kinawekwa katika mtandao.
SABA: Ni kutumia vibaya vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu bila kuzingatia muda muafaka wa kuonyesha vipaji vyao. Mfano mzuri ni wale waliojaaliwa kuimba yani muziki, wengi wao huanza kuwekeza muda wao mwingi katika muziki ilihali wakiwa wangali bado shule. Wengi wao huishia hapo walipofika kwani muziki ni mtamu sana na ustar (umaarufu) pia ni mtamu, hivyo huwezi kuwa star kwa mazingira yetu ya St. Kayumba na ukasoma na kufaulu vizuri. ANGALIZO - Wanafunzi wenye vipaji tunawahitaji sana katika sanaa lakini fanya sanaa yako pale unapohitajika, kwa mfano shuleni au chuo kuna mashindano ya kuchora wewe chora sana, kuna mashindano ya kuimba - onyesha umahiri wako, lakini baada ya hapo rejea katika mazingira ya kimasomo.
NANE: Mapenzi pia ni tatizo katika masomo, kumbuka mapenzi ni kitu nyeti na special sana ndio maana yakatengewa muda wake na umri pia. Kumbuka mapenzi na masomo ni mafuta na maji. Kwa hili wanafunzi inapaswa muwe makini nalo ili muweze kufanya vizuri katika masomo yenu.
TISA: Walimu wanapaswa kutoa ripoti ya mwanafunzi kila baada ya muda kwa mzazi wa mwanafunzi bila mwanafunzi kuhusishwa. Kwani mwanafunzi anapopewa ripoti yake yeye mwenyewe na inaonyesha maovu yake aliyofanya shuleni, si kweli kama ataifikisha salama nyumbani kwa mzazi wake.
KUMI na mwisho ni kwa mzazi wa mwanafunzi, wazazi wengi wa shule za international, English Mideum, Missionary na nyinginezo za wenye uwezo, hufuatilia kwa karibu ripoti za maendeleo ya wanawe bila kukosa, na tena wakikosa hulipishwa hata fine (tozo). Hivyo ni vyema wazazi wakafuatilia. maendeleo ya watoto wao wanapokuwa shuleni
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home