Saturday, April 1, 2023

Jumapili ya matawi

 ๐ˆ๐…๐€๐‡๐€๐Œ๐” ๐‰๐”๐Œ๐€๐๐ˆ๐‹๐ˆ ๐˜๐€ ๐Œ๐€๐“๐€๐–๐ˆ.


Jumapili ya matawi ni jumapili moja kabla ya sherehe ya ๐๐š๐ฌ๐š๐ค๐š ambayo kwa mujibu wa Injili, Kanisa Katoliki huanza ๐ฐ๐ข๐ค๐ข ๐ญ๐š๐ค๐š๐ญ๐ข๐Ÿ๐ฎ kwa lengo la kukumbuka mateso, kifo na ufufuko wa ๐๐ฐ๐š๐ง๐š wetu ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ ๐Š๐ซ๐ข๐ฌ๐ญ๐จ.


Pia ndiyo siku maalumu ambayo Wakristo wengi hukumbuka na kusherekea siku ile ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ alipoingia Yerusalemu kwa mara ya mwisho kama ๐Œ๐ฐ๐จ๐ค๐จ๐ณ๐ข na ๐Œ๐Ÿ๐š๐ฅ๐ฆ๐ž wao.


Inasemekana kuwa, siku hiyo ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ alipokuwa anaingia Yerusalemu alipanda punda huku umati mkubwa wa watu hasa vijana wakimfuata kwa furaha, wengine walishika matawi na kutandaza nguo zao chini ili kumpa ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ heshima ya Kifalme na kuimba:


"๐‡๐จ๐ฌ๐š๐ง๐š ๐Œ๐ฐ๐š๐ง๐š ๐ฐ๐š ๐ƒ๐š๐ฎ๐๐ข, ๐ง๐๐ข๐ฒ๐ž ๐Œ๐›๐š๐ซ๐ข๐ค๐ข๐ฐ๐š, ๐ฒ๐ž๐ฒ๐ž ๐š๐ฃ๐š๐ฒ๐ž ๐ค๐ฐ๐š ๐ฃ๐ข๐ง๐š ๐ฅ๐š ๐๐ฐ๐š๐ง๐š, ๐ก๐จ๐ฌ๐š๐ง๐š ๐ฃ๐ฎ๐ฎ ๐Œ๐›๐ข๐ง๐ ๐ฎ๐ง๐ข". (๐Œ๐š๐ญ๐ก๐š๐ฒ๐จ 21:1-11)


Neno la Mungu linatuambia kwamba, tukio hilo la kupunga matawi na mengine kuyatandaza chini ili ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ apite juu yake, basi matawi hayo yaliwakilisha mema na alama kubwa ya ushindi juu ya kifo alichokishinda Yesu baada ya siku tatu alipofufuka kaburini. (1๐–๐š๐ค๐จ๐ซ๐ข๐ง๐ญ๐ก๐จ 15:55)


Lakini pia kitendo cha ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ kupanda punda, ilikuwa ni kutimiza ule unabii uliotolewa tangu kale juu ya ufalme wake, maana nyakati zile Wafalme wa Kisraeli walipokuwa wakilakiwa na watu huwa wanapanda punda, huku wakiimbia nyimbo za kishujaa.


Kibiblia "๐๐ฎ๐ง๐๐š" huwakilisha amani, kwahiyo wale waliomlaki ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ, walionesha kujawa na amani, kwa kuwa walimuona ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ kama ๐Œ๐Ÿ๐š๐ฅ๐ฆ๐ž wao atakayeleta amani ndani ya taifa la Israeli.  (๐™๐ž๐ค๐š๐ซ๐ข๐š 9:9)


Kadhalika hata neno "๐‡๐จ๐ฌ๐š๐ง๐š" Kibiblia lilimaanisha "๐Ž๐ค๐จ๐š ๐ฌ๐š๐ฌ๐š",  hivyo Waisraeli walimwiimbia ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ wimbo huo wakiamini kwamba, muda si mrefu yule ๐Œ๐š๐ฌ๐ข๐ก๐š waliomgojea ataenda kuwaokoa dhidi ya ukatili, manyanyaso na dhuluma ya dola ya kirumi iliyokuwa inatawala nchi yao.


Ingawa Biblia inafunua wazi kuwa, japo Waisraeli walimuona ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ kama ๐Œ๐Ÿ๐š๐ฅ๐ฆ๐ž wao kwenye mambo ya siasa, kumbe ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ hakuja ulimwenguni kwa ajili hiyo, bali alikuja ili kutuokoa kutoka kwenye dhambi ya mauti na kifo, na hiyo ndiyo ilikuwa ajenda kuu ya utume wake alioufanya hapa duniani miaka 2000 iliyopita. (๐˜๐จ๐ก๐š๐ง๐ž 12:12-15, ๐™๐š๐›๐ฎ๐ซ๐ข 118:25-28 na ๐–๐š๐ซ๐ฎ๐ฆ๐ข 10:9)


Pia hata ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ alipokuwa anaukaribia mji, Biblia inatuambia kwamba aliulilia sana kwa machozi licha ya kushangiliwa kwa furaha na watu waliomzunguka. Maana alitambua kuwa, muda si mrefu wale wanaomshangilia ndio watakaomsaliti na kumuua kwa kifo cha aibu na maumivu makali pale Msalabani Kalvari. (๐‹๐ฎ๐ค๐š 19:41-42)


Hivyo nihitimishe kwa kusema kwamba, jumapili hii ya matawi itukumbushe kufahamu kuwa ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ ๐Š๐ซ๐ข๐ฌ๐ญ๐จ ndiye ๐Œ๐ค๐ฎ๐ฎ kuliko mtu yeyote yule duniani, na hii ndiyo sababu kuu ya kusherekea juma hili, kwani kupitia sadaka ya kifo chake pale Msalabani, sote tuliwekwa huru kutoka mauti na kuingizwa kwenye furaha ya uzima wa milele.


Basi ndugu zangu ๐˜๐ž๐ฌ๐ฎ tunayemshangilia leo, tukamshangilie siku zote katika maisha yetu kwa kutenda mema na kuacha maovu wala tusimsaliti kama vile Waisraeli walivyofanya, bali tuwe waaminifu kwa Mungu na jirani zetu, maana usaliti sio mzuri, inaweza kuondoa amani na kuleta machafuko pamoja na mauaji kwa wale wanaotuamini, hivyo tujifunze kupitia tukio hili la matawi ili tuishi vizuri na wenzetu.


๐€๐ฌ๐š๐ง๐ญ๐ž ๐ง๐š ๐Œ๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ ๐š๐ฐ๐š๐›๐š๐ซ๐ข๐ค๐ข...

Saturday, November 25, 2017

MLO MZULI KWA WAJAWAZITO

MLO MZULI KWA WAJAWAZITONa MICHAEL MATAHIMBA
Je mlo gani ni bora kwa mama mjamzito ?
Kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama mtarajiwa anatakiwa kupata mlo ulio kamili kwa muda sahihi na kiwango kinachotakiwa. Mlo kamili hutokana na vyakula mchanganyiko kutoka kwenye makundi yote muhimu ya vyakula. Kwenye makala yetu ya leo tunaangalia vyakula muhimu kwenye kujenga afya ya mama na mtoto anayekua tumboni.
Kupata mlo kamili huhakikisha mama anapata virutubisho vyote muhimu na kwenye kiwango sahihi kwa mahitaji yake na mtoto anayekua. Njia rahisi ya kuapta mlo sahihi ni kupata kiwango kinachotakiwa cha chakula kutoka katika kila kundi la vyakula. Umuhimu wa lishe bora ni kuufanya mwili kuongezeka uzito, kuzuia upungufu wa damu, kuboresha ukuaji na maendeleo ya mtoto aliyepo tumboni. Yafuatayo ni makundi tofauti ya virutubisho vya chakula yanayotakiwa kupewa kipaumbele kwenye mlo wa mama mjamzito.
1. Vyakula vya wanga ( kabohaidreti)
Wanga ni chanzo kikubwa cha nguvu mwilini. Vyakula vya wanga vimegawanyika katika makundi matatu wanga, sukari na ufumwele. Vyakula hivi hupatikana kwa wingi na kwa urahisi zaidi kwenye nafaka kama mahindi,mchele, mtama, ulezi na ngano. Vilevile, vyakula hivi hupatikana kwenye vyakula vya mizizi kama mihogo, viazi vikuu, magimbi na viazi vitamu.
Vyakula hivi huusaidia mwili wa mama kutengeneza mafuta, kuupa mwili joto na nguvu.
Ukosefu wa vyakula hivi huusababisha mwili kukosa mafuta, kudhoofika kwa nyama za mwili na kupungua uzito.
2. Vyakula vya wanyama (Dairy)
Vyakula vinavyotokana na wanyama kama mayai au maziwa vina virutubisho muhimu sana kwa mama mjamzito. Mama anapata vitamin, madini na virutubisho vingi sana kutoka kwenye maziwa. Kwenye maziwa yanapata madini ya Calcium ambayo husaidia ukuaji wa mifupa ya mtoto.
Vilevile kuna protini, vitamin D na phosphorus. Ieleweke kuwa mama mjamzito anahitaji protini asilimia 60 zaidi ya kiwango anachohitaji mama asiye mjamzito.
3. Jamii ya kunde
Vyakula hivi ni vyanzo vya protini, ufumwele na vitamin kwa wingi. Ni vyakula ambavyo havigharimu fedha nyingi na vinapatikana kwa wingi. Maharage yana kiwango kikubwa sana cha protini ambayo hutumika mwilini moja kwa moja bila kuleta madhara zaidi mwilini.
4. Mafuta
Vyakula vyenye mafuta ni kama vile alizeti, nazi, mawese, omega 3 na mbegu zinazotoa mafuta. Mafuta yakiongezwa kwenye chakula huboresha usharabu wa baadhi ya vitamin na huongeza kiasi cha nishati. Kuna baadhi ya samaki wana mafuta yenye uwepo wa virutubisho vya omega-3 ambavyo husaidia kuboresha ubongo, hasa wa mtoto anayekua. Virutubiosho hivi pia hupatikana kwenye mayai ya kuku wa kienyeji.
Mafuta haya humsaidia binadamu kua na uwezo mkubwa wa kufikiria na kutunza kumbukumbu. Pia mafuta husaidia mtoto kuzuia magonjwa kama autism, kisukari. Pia ni kinga nzuri kwa mama kwenye kuzuia kifafa cha mimba.
Mama mjamzito anatakiwa kupata gramu 250 za mafuta kila Siku kwa kipindi cha mwisho cha ujauzito. Hii itasaidia kujenga ubongo na mfumo wa fahamu wa mtoto

NJIA 13 ZA KULALA VIZURI USIKU

Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri

Kulala
Usingizi wa uhakika ni jambo jema sana kwa ajili ya afya ya mwili wako. Lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na kujengeka kwa jamii yenye mfumo wa maisha wenye shughuli nyingi, watu wengi hawapati usingizi mzuri.
Namkumbuka rafiki yangu mmoja alipata kazi nyingi sana kwenye mtandao. Hivyo ikamlazimu azifanye zote kwa muda mfupi bila kulala wala kula ipasavyo. Matokeo yake ameugua kwa miezi minne sasa na bado afya yake haijaimarika kama awali.
Hili linatupa umuhimu wa kuchunguza ni nini hasa manufaa ya kulala au usingizi mzuri?
  • Huimarisha na kuboresha ukuaji wa mwili.
  • Hujenga na kuimarisha kinga mwili.
  • Hukuweka katika hali nzuri (mood).
  • Hukuongezea kumbukumbu.
  • Hurefusha maisha.
  • Huboresha tendo la ndoa.
  • Huondoa msongo wa mawazo.
Haya ni baadhi tu ya manufaa ya kulala vyema; je huoni kuwa unahitaji kufahamu njia zitakazokupa usingizi au kulala vyema? Fuatana nami katika makala hii ili nikujuze zaidi.

1. Punguza mwanga wa rangi ya bluu jioni na usiku

Mwanga huu hupatikana hasa katika vifaa vya kielektroniki kama simu; kompyuta, televisheni n.k. Utafiti unaonyesha kuwa mwanga huu wa bluu hupunguza uzalishaji wa homoni ya โ€œmelatoninโ€ ambayo ndiyo hutupa usingizi.
Inashauriwa kuepuka kutumia mitandao ya kijaamii au kutazama vitu katika vifaa tajwa hapo juu usiku ili kuboresha usingizi wako.

2. Kaa kwenye mwanga wa kutosha mchana

Unapokaa kwenye mwanga wa kutosha mwili wako utaweza kutambua ni wakati upi umeamka na ni wakati gani wa kulala. Yaani mwili utatengeneza mazoea ya kubaini kuwa sasa ni usiku na ni wakati wa kulala kwani mchana kutwa hukuwa umelala.

3. Epuka matumizi ya caffeine jioni au usiku

Sokoni leo vipo vinywaji kadha wa kadha vilivyotengenezwa au kuongezewa caffeine. Matumizi caffeine huamsha na kuchangamsha mwili wako na kuuweka katika hali ya kutojipumzisha.
Hivyo matumizi ya caffeine jioni au usiku yatakupelekea kutopata usingizi mzuri. Vinywaji vyenye caffeine nyingi ni kama vile kahawa pamoja na baadhi ya soda Mf. Energy drink.

4. Punguza au acha kulala mchana

Mara ngingi unapolala mchana ni sawa na kusema umepunguza usingizi wa usiku. Kama siyo lazima kulala mara kwa mara mchana, basi ni vyema ukajitahidi kutolala ili kukupa usingizi wa uhakika na wa kutosha wakati wa usiku. Kumbuka, hakuna sababu ya kulala mchana wakati una usiku mzima wa kulala.

5. Zingatia ratiba ya kulala na kuamka

Natumaini umewahi kulala zaidi ya muda uliozoea kuamka; na ulipoamka ulijihisi umechoka sana. Vivyo hivyo kwa siku uliyochelewa kulala pia. Hivyo basi, jitahidi kulala na kuamka kwa wakati unaofanana ili mwili wako uweze kufuata utaratibu ambao umeuzoea.
Mwili unapobadilishiwa utaratibu wa kulala uliouzoea mara kwa mara ni dhahiri utakuonyesha matokeo hasi.

6. Usitumie kilevi/pombe

Kama nilivyoeleza katika hoja ya kwanza, โ€œmelatoninโ€ ni homoni muhimu inayotuwezesha kulala. Utafiti uliofanyika umebaini kuwa uzalishaji wa homoni hii huathiriwa sana na matumizi ya pombe.
Pombe ni kinywaji ambacho kimeonyesha kuwa na hasara nyingi katika mwili wa binadamu, hivyo ni vyema ukajitahidi kuepuka matumizi ya pombe.

7. Boresha mazingira ya chumba unacholala

Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wanaopata matatizo ya kulala yanasababishwa na mazingira mabaya ya vyumba vyao vya kulala. Hakikisha unalala kwenye chumba ambacho hakina mwanga mwingi, joto kali, baridi, uhaba wa hewa au kelele.
Mambo unayoweza kufanya ili kuboresha chumba chako:
  • Zima au punguza mwanga katika  chumba chako.
  • Zima redio, televisheni au kifaa kingine kinachosababisha kelele.
  • Fungua madirisha ili kuhakikisha unapata hewa yakutosha.
  • Tawala joto  na baridi kwani visipokuwa vya wastani hutoweza kulala vyema โ€“ angalau nyuzi joto 20 zinatosha.
Naamini ukizingatia haya utaboresha chumba chako na kukuwezesha kulala vyema.

8. Usile sana usiku au usile vyakula vizito usiku

Kutokana na watu wengi kuwa na shughuli nyingi wakati wa mchana hushindwa kula vyema mchana; hivyo wanapendelea kula sana usiku.
Hili si jambo zuri kwani mwili unakuwa umepumzika wakati wa usiku; hivyo kula sana au kula vyakula vigumu kutapelekea mwili kutumia nguvu kubwa kumengโ€™enya chakula hicho. Ndiyo maana watu wengi wanaopendelea kula sana usiku huamka asubuhi wakiwa wamechoka sana.

9. Pumzisha na safi akili yako jioni

Kuna umuhimu wa kusoma au kusikiliza vitu vyenye kuburudisha na kuliwaza akili yako jioni kwani kutafanya akili yako kukuruhusu kupata usingizi wa uhakika.
Mambo ya kufanya katika hoja hii:
  • Epuka kutazama au kusikiliza filamu (Movies) au masimulizi ya kutisha (Hili litakuondolea maruweruwe na mangโ€™amungโ€™amu usiku).
  • Sikiliza mziki wa taratibu (slow music) kwa sauti ndogo jioni au usiku.
  • Soma vitabu vyenye maandiko ya kuliwaza na kuburudisha (Kama vile vitabu vya dini).
Naamini ukizingatia mambo haya utaweka akili yako katika hali nzuri ya kukupa usingizi wa uhakika.

10. Oga jioni au kabla ya kulala

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa, kuoga jioni au usiku kabla ya kulala, kutauweka mwili wako katika hali nzuri kiafya na kukufanya kulala vyema. Hivyo unaweza kuoga kabla ya kulala ua hata kusafisha miguu yako kwa maji kabla ya kulala ili kukuwezesha kupata usingizi mzuri.

11. Tumia godoro na mto bora

Watu wengi hujiuliza ni kwa nini huwa wanalala vyema kwenye hoteli kuliko nyumbani kwao. Jibu ni kutokana na kutumia godoro na mto bora zaidi kuliko ule wanaoutumia nyumbani kila siku.
Godoro duni na mto duni vitakusababishia maumivu ya shingo na ya uti wa mgongo hivyo kusababisha usilale vyema. Jitahidi kuhakikisha unanunua na kutumia godoro na mto ulioidhinishwa na wataalamu.

12. Fanya mazoezi; lakini si kabla ya kulala

Mazoezi ni muhimu kwa ajili ya kujenga na kulinda afya ya mwili wako. Jitahidi kuwa mtu anayefanya mazoezi mara kwa mara kwani kutakuongezea uwezo wa kulala vyema wakati wa usiku; kwa kuwa mwili utajipumzisha vyema ili kujijenga tena.
Faida za mazoezi:
  • Hupunguza athari za magonjwa
  • Hupunguza uzito
  • Huongeza ujasiri
  • Huimarisha mwili
  • Hukuwezesha kulala vyema
  • Huongeza kumbukumbu
  • Huongeza furaha
  • Huongeza uwezo wa kujiamini

13. Usinywe vimiminika kwa wingi usiku

Maji ni muhimi kwa ajili ya afya yako, lakini unywaji wa maji mengi au vimiminika wakati wa usiku si jambo jema kiafya. Kunywa maji au vimiminika kwa wingi usiku kutakusababisha kuamka mara kwa mara kwenda uwani; hivyo utakuwa na usingizi unaokatishwa katishwa mara kwa mara.
Ni vyema kujijengea mazoea ya kunywa maji au vimiminika kidogo usiku au ikibidi kunywa kwa wingi basi vinyweke mapema.
Hitimisho
Zilizojadiliwa hapa ni njia zitakazokuwezesha kupata usingizi mzuri. Ni dhahiri kuwa kukosa usingizi mzuri hutokana na utaratibu mbaya wa maisha ambao mtu amejiwekea. Hivyo basi, badilika, kabla ya mambo yote jali kwanza afya yako ili uweze kuwa na tija zaidi.

FAIDA ZA KUNJWA MAZIWA


Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Faida za maziwa
Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa?
Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa.

1. Hujenga na kulainisha ngozi

Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara.
Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.

2. Huimarisha meno

Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D.

3. Huimarisha mifupa

Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao. Ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa (osteoporosis). Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D.

4. Kujenga misuli

Maziwa yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena. Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali.

5. Kupunguza uzito

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda. Pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula yaani appetizer.

6. Huondoa msongo wa mawazo

Hebu fikiri juu ya vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziwa; hivi huweza kuondoa msongo. Baada ya kazi nyingi za siku, inashauriwa kunywa angalau bilauri (glass) moja ya maziwa ya uvuguvugu. Hili litakusaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu.

7. Huzuia maumivu wakati wa hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

8. Huongeza nguvu za mwili

Je unaishiwa nguvu mapema au kuchoka sana? Kama jibu ni ndiyo, unahitaji virutubisho vilivyoko kwenye maziwa. Hivi vitaupa mwili wako nguvu mpya na kukufanya kuwa mwenye nguvu na furaha siku nzima.

9. Huondoa kiungulia

Kiungulia huwasumbua sana watu wengi. Kiungulia husababishwa na asidi zipatikanazo tumboni. Hivyo maziwa (ambayo si mgando) hutengeneza utando maalumu tumboni ambao hupambana na asidi hizi.
Kwa hiyo nywaji wa maziwa (ambayo si mgando) utakusaidia kupambana na tatizo la kiungulia ndani ya muda mfupi.

10. Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.
Hitimisho
Yaliyozungumziwa hapa ni faida 10 za kunywa maziwa. Naamini umebaini kuwa maziwa yana manufaa mengi sana kwa ajili ya afya yako zaidi ya haya yaliyotajwa. Ni jambo jema kujizoesha kula vitu vya asili, kwani ndivyo huhitajiwa zaidi na mwili wa mwanadamu. Jizoeze kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili wako.

VYOMBO VYA PLASTIC VINA ATHALI


Athari 5 za Kutumia Vyombo vya Chakula vya Plastiki

Vyombo vya plastiki
Plastiki ina nafasi kubwa kwenye jamii ya leo; hutumika kwenye magari, vyombo vya nyumbani, vifaa vya watoto vya kuchezea, simu, kompyuta n.k. Kwa hakika siyo rahisi mtu kumaliza siku nzima bila kutumia kifaa chochote cha plastiki.
Pamoja na nafasi hii kubwa ya matumizi ya plastiki, plastiki imekuwa na athari mbalimbali kwenye afya ya binadamu pamoja na mazingira.
Karibu nikufahamishe madhara au athari 5 zitokanazo na matumizi ya vifaa au vyombo vya chakula vilivyotengenezwa kwa plastiki.

1. Sumu zilizoko kwenye plastiki zinaweza kukufanya uugue

Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa sumu zilizoko kwenye vifaa vya plastiki zinaweza kusababisha maradhi kama vile saratani, maradhi ya kupoteza kumbukumbu, maradhi ya moyo pamoja na kupoteza uwezo wa kuona.
Wataalamu mbalimbali walisisitiza kuwa sumu hizi huyeyuka na kuingia mwilini hasa pale vyombo vya plastiki vinapowekwa vyakula au vinywaji vya moto.

2. Plastiki huathiri afya ya uzazi

Inaelezwa kuwa kemikali kama vile Bisphenol A inayopatikana kwenye vyombo vingi ya plastiki, ina madhara makubwa kwenye afya ya uzazi.
Watafiti wanaeleza kuwa kemikali hii huathiri uzalishaji wa homoni, ukuaji wa watoto pamoja na kusababisha tatizo la kutoka kwa mimba.

3. Hakuna plastiki salama

Mara nyingi baadhi ya wazalishaji wa vifaa vya plastiki hunadi bidhaa zao kwa kueleza kuwa hazina kemikali ya Bisphenol A (BPA), lakini vinaweza kuwa na kemikali nyingine ya Bisphenol S (BPS) ambayo sifa zake zinakaribiana na za BPA.
Hivyo ni muhimu kuwa makini au kuepuka matumizi ya plastiki kwenye chakula kwani watengenezaji wengi siyo waaminifu wala wa kweli.

4. Huongeza unene

Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa matumizi ya vyombo vya chakula vilivyotengenezwa kwa plastiki huongeza unene wa mwili. Hili ni kutokana na kemikali zinazopatikana kwenye plastiki ambazo hubadili seli shina (stem sell) kuwa seli za mafuta.
Inaelezwa pia kemikali za plastiki zikiingia mwilini huingilia mchakato wa metaboli mwilini na kufanya kalori zikusanyike mwilini badala ya kutumika na kuondoka.

5. Huharibu mazingira


Chazo cha picha: Idogs.in
Ngโ€™ombe wakila mifuko ya plastiki kutokana na uchafuzi wa mazingira.

Ni wazi kuwa vyombo vya chakula au vinywaji vinapokwisha muda wake hutupa kwenye mazingira yanayotuzunguka. Swala hili huathiri viumbe na mimea mbalimbali.
Plastiki zinapokuwa katika mazingira huathiri ukuaji wa mimea, huweza kuliwa na wanyama pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji.

ndege
Chanzo cha picha: Publicbroadcasting.net
Ndege aliyekufa akiwa amemeza vipande vya vitu mbalimbali vya plastiki.

Neno la mwisho
Ni ukweli suiopingika kuwa plastiki zina matumizi makubwa lakini pia zina athari kubwa kwenye afya zetu na mazingira. Ni vyema ukatumia vyombo vya udongo, kioo, mbao au hata vya alminiamu badala ya plastiki.
Ni muhimu kukumbuka kuwa maradhi mengi hutokana na sumu mbalimbali zinazoingia kwenye miili yetu. Pia ni muhimu kujali uhai na usalama wa vizazi vijavyo kwa kutunza mazingira ili yatutunze.

Madhara 12 ya Pombe Kiafya

Pombe
Siyo siri kuwa pombe husababisha matatizo makuwa ya kiafya, yakiwemo magonjwa ya moyo, ini pamoja na majeraha yatokanayo na ajali zitokanazo na ulevi. Ni dhahiri kuwa vinywaji halisi vilivyotengenezwa kwa matunda bila kilevi ni bora zaidi kwa afya yako kuliko vile vyenye kilevi.
Licha ya kuwepo kwa kampeni kadha wa kadha zinazopinga matumizi ya pombe, bado watu wengi wameendelea kushikilia kinywaji hiki bila kufahamu athari zake kwenye afya zao. Fuatilia hapa chini athari 12 za pombe kiafya.

1. Matatizo ya moyo

Unywaji mkubwa wa pombe husababisha  matatizo mbalimbali ya moyo kama vile cardiomyopathy, ambapo mishipa ya moyo hudhoofika na kushindwa kusukuma damu. Jambo hili huweza kusababisha damu kuganda na kusababisha kiharusi (stroke). Pombe huchangia sana katika kudhoofisha mishipa ya moyo hivyo kupelekea ugonjwa huu wa cardiomyopathy na mengine hatari.

2. Tatizo la ini

Unywaji wa pombe unaweza kusababisha maradhi ya ini yajulikanayo kama Cirrhosis; ambayo ni maradhi ya ini kushindwa kufanya kazi yake kutokana na uharibifu wa muda mrefu. Uharibifu huu husababisha seli za ini kuwa makovu na kushindwa kufaya kazi vyema. Utafiti umebaini kuwa pombe huchangia sana katika kuharibu seli hizi za ini.

3. Shinikizo la damu

Unywaji wa pombe hasa kupitiliza umedhibitishwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maradhi ya shinikizo la damu. Imebainikia kuwa pombe huathiri mfumo wa usukumaji wa damu mwilini jambo ambalo hupelekea shinikizo la damu na baadye matatizo mengine kama kushindwa kwa figo, ini n.k.

4. Magonjwa ambukizi

Mara nyingi mtu anapokunywa pombe hupoteza uwezo wa kutawala mwili na maamuzi yake. Hivyo ni rahisi baada ya mtu kunywa pombe akafanya au akajiingiza kwenye matendo hatarishi yanayoweza kumfanya kuambukizwa magonjwa kama vile UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.

5. Ugonjwa wa anemia

Anemia ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kwa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha kwenda kwenye mwili. Hivyo unywaji wa pombe hupunguza uwezo wa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni ya kutosha hivyo kupelekea ugonjwa wa anemia.

6. Saratani

Utafiti uliofanywa na daktari Jurgen Rehm, PhD, wa chuo cha Toronto umebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani kutokana na unywaji wa pombe. Utafiti huu ulieleza kuwa tatizo huanza pale ambapo mwili hubadili kilevi (alcohol) kuwa kemikali iitwayo โ€œacetaldehydeโ€.
Saratani huweza kutokea kwenye koo, shingo, mdomo na mapafu. Pia aliongeza kuwa atari inaongezeka pale ambapo mtumiaji wa pombe pia ni mvutaji wa sigara.

7. Kusinyaa kwa ubongo

Kadri umri wa mtu unavyozidi ndivyo na ubongo wake unavyozidi kusinyaa. Hivyo unywaji wa pombe huharakisha kusinyaa kwa ubongo kwa silimia 1.9. Hili hupelekea matatizo yatokanayo na kusinyaa kwa ubongo kama vile kupoteza au kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu.

8. Msongo wa mawazo

Pombe huathiri mchakato wa kikemikali wa ubongo (Kemia ya ubongo). Kutokana na utafiti uliofanywa, imebainika kuwa watu wanaokunywa pombe nyingi hukabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Msongo wa mawazo ni chanzo cha maradhi mbalimbali kama vile shinikizo la damu, matatizo ya akili, matatizo ya moyo na wakati mwingine kifo.

9. Maumivu ya miguu (gout/jongo)

Gout au jongo ni ugonjwa wa miguu unaotokana na kukusanyika kwa asidi kwenye viungio vya mifupa. Mara nyingi ugonjwa huu hujitokeza sana majira ya baridi. Pamoja na vyanzo vya sababu za kurithi za ugonjwa huu, pombe imedhihirika kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ugonjwa huu.

10. Uharibifu wa mfumo wa fahamu

Hivi leo pombe mbalimbali hutengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali, kemikali hizi kwa kiasi kikubwa huwa na athari kwenye mfumo wa fahamu. Pombe huathiri mifumo na utendeji kazi wa mfumo mzima wa fahamu na kusababisha matatizo kama vile udhaifu wa misuli na matatizo katika milango la fahamu.
Hii ndiyo sababu mtu anayekunywa pombe kali anashindwa kuhisi landa za vitu kama vile chumvi au pilipili vyema; hivyo hujikuta akitumia kwa kiasi kikubwa.

11. Kusinyaa kwa uso na macho

Unywaji mkubwa wa pombe husababisha kusinyaa kwa uso na macho hasa kwa wale wanaokunywa usiku. Mara ngingi uwatazamapo wanywaji wakubwa wa pombe utaona hata sura zao zimebadilika na kuonekana zimezeeka au kuchoka kuliko awali.
Ni dhahiri umewahi kumwona kijana mlevi wa miaka 25 lakini anaonekana kama mzee wa mika 40. Hii ni kutokana na athari zinazosababishwa na unywaji mkubwa wa pombe.

12. Huathiri mifumo ya uzazi

Kumekuwa na mawazo kadha wa kadha kuhusu pombe na maswala ya uzazi. Wengine huamini kuwa pombe huboresha maswala ya uzazi huku wengine wakiamini kuwa pombe huathiri maswala ya uzazi. Ukweli ni kuwa pombe ina madhara kadha wa kadha kwenye maswala ya uzazi kama ifuatavyo:
  • Husababisha kukutana kimwili kusiko salama.
  • Huathiri nguvu za kiume.
  • Huathiri mtoto aliye tumboni kwa mama.
  • Husababisha watu kufanya matendo binafsi au ya aibu hadharani.
Je bado unatamani kuendelea kukumbatia pombe katika maswala ya uzazi? Naamini utafanya uamuzi sahihi sasa.
Neno la Mwisho
Maamuzi ya kujenga au kubomoa maisha yako kutokana na pombe ni ya kwako. Naamini umefahamu madhara kadha wa kadha ya pombe kiafya. Kumbuka kuwa yapo pia madhara ya kijamii, kiuchumi na hata kiimani kwa wale waaminio.
Usauri wangu kwako ni kuwa hakuna mtu aliyewahi kufa kutokana na kuacha kutumia pombe. Hivyo jenga mwili wako kwa lishe bora ili uwe mwenye tija zaidi.